Nasa kwa haraka ubao mweupe, telezesha au weka waraka. OneNote itaupunguza na kuuboresha ili uwe rahisi kusoma. Pia tutatambua matini yaliyocharazwa, kwa hivyo unaweza kuuangalia baadaye.
Chora mchoro kutoka kwenye ubao kwa kalamu. Andika vidokezo vyako vyote kwa mkono iwapo utagundua kuwa ni asili kuliko kucharaza.
Usiandike chini kila neno kutoka kwa mhadhiri andika sehemu muhimu pekee. OneNote huunganisha vidokezo vyako kwenye sauti, kwa hivyo unaweza kuruka moja kwa moja kwa jambo lililokuwa likisemwa ulipoandika kila kidokezo.
OneNote ilibuniwa kuwa haraka na rahisi kubadilika kwa matini, orodha na majedwali ya mambo ya kufanya. Usijali kuhusu miundo, andika mahali popote kwenye ukurasa unaotaka.
Iwapo una barua pepe yao, unaweza kushiriki nao. Ni rahisi na haraka kuanza.
Iwapo mko kwenye chumba sawa au kwenye chuo, fanyeni kazi pamoja kwa muda halisi. Alama za usahihishaji hukufahamisha anayefanyia kitu fulani kazi.
Darasani, chumbani mwako, kwenye maabara ya kompyuta au kwenye mkahawa mnaweza kufanya kazi pamoja kutoka mahali popote kwenye kifaa chochote. OneNote hulandanisha kiotomatiki ili kukuwekea mambo pamoja, hata iwapo mtu ataondoka mtandaoni.
Utafiti wa wavuti ni muhimu kwenye miradi mingi. Nasa ukurasa wowote wa wavuti kwenye kivinjari chochote kwa mbofyo mmoja. Fafanua ukurasa kwenye OneNote.
Weka slaidi na makaratasi ya mhadhiri kwa vidokezo vyako. Andika vidokezo juu au kando yake kwa kucharaza au kuandika kwa mkono kwa kalamu yenye ncha.
Andika juu ya picha au nakala. Panga kama vidokezo vya kubandika, ili kuleta dhana ya hoja zako. Toa maoni kwa kuandika kwenye pambizo tu.
Je, ni mratibishaji au piler? OneNote huzipenda zote. Weka vidokezo na miradi yako kwa mpangilio kwa kuunda madaftari na sehemu. Tafuta na upate kwa urahisi matini yoyote uliyoyachapisha, kubana, na kuandika kwa mkono.