Chagua daftari chaguo-msingi na sehemu ambayo barua pepe zitahifadhiwa.
Maudhui ya barua pepe
Tuma barua pepe kwa me@onenote.com ili kuihifadhi moja kwa moja katika OneNote. Unaweza kuzifikia barua pepe ulizohifadhi katika OneNote kutoka kwenye kifaa chako chochote.
Uthibititishaji wa Safari
Fuatilia mipango ya safari zako zijazo katika OneNote kwa kusambaza barua pepe zako za uthibitisho wa ndege na hoteli.
Dokezo la haraka kwako mwenyewe
Andika wazo au kazi ya baadaye na uihifadhi kwenye OneNote.
Stakabadhi
Hifadhi stakabadhi za ununuzi wa mtandaoni ili kurahisisha kuzipanga na kuzipata.
Barua pepe muhimu
Hifadhi barua pepe ambayo huenda ukataka kurejelea baadaye kutoka kwenye kifaa kingine.
Maswali Yanayoulizwa Sana
Ninaweza kutuma barua pepe kutoka anwani ya barua pepe isiyo ya Microsoft?
Ndiyo, unaweza kuongeza anwani yoyote ya barua pepe unayomiliki kwenye akaunti yako ya Microsoft na kuiwezesha kwa kipengele hiki.
Barua pepe zangu zinahifadhiwa wapi?
Unaweza kubadilisha eneo lako la kuhifadhi chaguo-msingi kwenye Ukurasa wa mipangilio. Pia unaweza kuchagua sehemu tofauti ya kuhifadhi barua pepe ya binafsi kwa kujumuisha alama ya "@" ikifuatiwa na jina la sehemu katika kichwa cha barua pepe yako.