Programu Zilizoangaziwa
Pata zaidi kutokana na OneNote kwa programu na vifaa hivi.
Brother Web Connection
Mashine yako ya Brother (MFP/Kitambazaji cha waraka) yanaweza kutambaza taswira na kuzipakia kwenye OneNote na OneDrive moja kwa moja bila kupitia kwenye PC.
Chegg
Wanafunzi wanaweza kuhifadhi majibu muhimu ya kazi yao ya nyumbani kutoka Chegg Study Q&A hadi OneNote. Ni rahisi kwa kitufe cha OneNote "Ibane". Kutoka hapo, unaweza kuanza kupanga majibu yako kwa mada, darasa au zoezi na kuweza kuyatafuta papo hapo kwenye OneNote. Unda mwongozo wa mwisho wa utafiti na ushirikina wanafunzi wenzako.
cloudHQ
Unganisha matini ya OneNote pamoja na cloudHQ. Landanisha madaftari yako pamoja na huduma nyingine maarufu za wingu kama vile Salesforce, Evernote, Dropbox. Shirikiana na wengine kwa urahisi, shiriki mawazo yako katika programu yoyote, na uyalandanishe kiotomatiki kwenye OneNote. Pia cheleza madaftari yako ya OneNote katika huduma nyingine za wingu ili kulinda mawazo yako endapo utayafuta kwa kutokusudia.
Newton
Hifadhi barua pepe muhimu kwenye OneNote kwa kubofya tu ukitumia Newton. Iwe ni ankara, stakabadhi, au barua pepe muhimu ya mteja, tumia ujumuishaji wa Newton's OneNote kuweka kila kitu pamoja.
Docs.com
Docs.com huwaruhusu watumiaji kusambaza madokezo au nyenzo za kujifunza kupitia madaftari ya OneNote. Huwezesha watu kama walimu na wanafunzi kote ulimwenguni kutazama na kutumia tena daftari lako la OneNote, na kuongeza umaarufu na ushawishi katika jamii.
Doxie Mobile Scanners
Doxie ni aina mpya ya kitambazaji karatasi kinachochajiwa upya, kwa hivyo unaweza kutambaza nyaraka mahali popote - hakuna kompyuta inayohitajika. Ichaji tu na uiwashe, popote ulipo - ingiza karatasi, risiti, na picha zako za kutambaza, kuhifadhi kwenye kumbukumbu, na kushiriki. Doxie hutambaza kila mahali, na kisha hulandanisha kwenye OneNote kwa ufikiaji kwenye nyaraka zako zote zilizotambazwa, kwenye vifaa vyako vyote
EDUonGo
EDUonGo huruhusu yeyote kuanzisha akademia au kozi ya mtandaoni kwa dakika chache. Wanafunzi wa EDUonGo wanaweza kuhamisha vipindi kwa urahisi kwenye madaftari yao. Hili linarahisisha wanafunzi kuunda matini na kushiriki na wengine. Wanafunzi pia wanaweza kuunganisha akaunti zao za OneDrive. Kama walimu, unaweza kujumuisha video kutoka Office Mix katika vipindi vyako.
Tuma Barua pepe kwa OneNote
Nasa mambo ambayo ni muhimu kwako popote ulipoi kwa kuyatuma kwa barua pepe moja kwa moja kwenye daftari lako! Tuma nyaraka, vidokezo, taratibu, na mengine zaidi kwenye me@onenote.com na tutayaweka kwenye daftari lako la OneNote, ambapo unaweza kuyafikia kutoka kwenye vifaa vyako vyote.
Epson Document Capture Pro
Document Capture Pro hukuruhusu kutambaza nyaraka, kuhariri kurasa, kuhifadhi faili, na kuhamisha data kwa urahisi kwenye programu zilizotambazwa kwa vitambazaji vya Epson kama vile Workforce® DS-30, DS-510, DS-560 na vingine. Kilicho cha ziada, watumiaji wanaweza kutambaza kwenye OneNote kwa mguso mmoja, ili kufikia kwa urahisi nyaraka kutoka kwenye vifaa anuwai au kushiriki na wengine.
eQuil Smartpen2 & Smartmarker
Andika madokezo yako kwenye sehemu yoyote na uyatume kwenye OneNote kwa kuifanya kuwa sehemu mahiri yenye eQuil Smartpen2 na Smartmarker. Ni njia ya kawaida ya kunasa mawazo bora zaidi.
Feedly
Feedly huunganisha visomaji kwa taarifa na maelezo wanayopenda. Tumia feedly kugundua na kufuata maudhui makuu, kisha hifadhi makala bora zaidi moja kwa moja kwenye OneNote kwa mbofyo mmoja.
Paper na Pencil na FiftyThree
Nenda kutoka kwenye Pencil hadi Paper kwa mawazo yako kisha uipeleke hatua moja zaidi ukitumia OneNote. Andika na uchore kwa Pencil rahisi na yenye uhakika ulioboreshwa unaojulikana kwayo, na ukikosea geuza tu sindano ya simu na ufute kwa njia ya kawaida - yote moja kwa moja katika OneNote. Andika madokezo kwa urahisi, unda orodha hakikishi na uchore katika Paper kisha ushiriki kwenye OneNote ili ufanye zaidi, kama vile kufanya kazi pamoja katika daftari lililoshirikiwa, na katika rekodi za sauti na ufikie maudhui yako kutoka kwenye karibu kifaa chochote.
Genius Scan
Genius Scan ni kitambazaji ulicho nacho. Hukuwezesha kuandaa nyaraka za karatasi kidijitali, kuunda faili za PDF na kuzihifadhi mara moja kwenye OneNote.
JotNot Scanner
JotNot hugeuza iPhone yako kuwa kitambazaji bebezi cha kurasa anuwai. Unaweza kutumia JotNot kutambaza nyaraka, risiti, bao nyeupe, kadi za biashara na vidokezo kwenye umbizo la kielektroniki. JotNot sasa hutoa muunganisho wa moja kwa moja kwa mfumo wa OneNote wa Microsoft, ili uweze kucheleza kwa haraka na rahisi na kupanga utambazaji wako kwa kutumia akaunti ya OneNote.
Livescribe 3 Smartpen
Ukiwa na programu ya Livescribe 3 smartpen na Livescribe+, andika tu kwenye karatasi na utazame kila kitu kikionekana papo hapo kwenye kifaa chako cha mkononi, mahali unaweza kuweka lebo, kutafuta na kugeuza vidokezo vyako kuwa matini. Unaweza kutuma kila kitu kwenye OneNote ili vidokezo na michoro yako iliyoandikwa kwa mkono iunganishwe kwa maelezo yako mengine muhimu.
Mod Notebooks
Mod ni daftari la karatasi linalofikiwa kutoka kwenye wingu. Andika vidokezo kwa kalamu na karatasi linalofahamika, kisha kurasa zako zitafanywa dijitali bila malipo. Kila ukurasa wa daftari kamilifu unaweza kulandanishwa kwenye OneNote na uhifadhi milele.
NeatConnect
NeatConnect hubadilisha mirundiko ya karatasi hadi kwenye nyaraka za dijitali na kuzituma moja kwa moja kwa OneNote - bila kompyuta. Kutoka kwenye chumba chochote nyumbani kwako, au eneo lolote afisini, upatanifu wa Wi-Fi wa NeatConnect na kiolesura cha skrini mguso hufanya utambazaji kwenye OneNote haraka na rahisi ili uweze kuokoa muda, kuendeleza shirika na uzalishaji hadi viwango vipya kabisa.
News360
News360 ni programu ya habari ya bila malipo iliyobinafsishwa inayofahamu unachopenda na inaboreka zaidi kadri unavyoitumia. Ikiwa na zaidi ya vyanzo 100,000, kila mara kuna jambo la kuvutia la kusoma, na unaweza kuhifadhi taarifa zako unazopenda moja kwa moja kwenye OneNote kwa mguso wa kitufe.
Nextgen Reader
Kisomaji cha RSS kilicho na kasi, safi na maridadi kwa Windows Phone. Sasa hukuwezesha kuhifadhi moja kwa moja kwenye OneNote. Furahia usomaji!
Office Lens
Office Lens ni kama kuwa na kitambazaji karibu nawe. Usikose kamwe vidokezo kwenye ubao mweupe au ubao mweusi, na usitafute kamwe nyaraka au kadi za biashara zilizopotea, risiti zinazokosekana au vidokezo potovu vya kubandika tena! Office Lens hufanya picha yako kusomeka kimaajabu na kutumika tena. Nasa maudhui moja kwa moja kwenye OneNote kwa upunguzaji na usafishaji otomatiki.
OneNote For AutoCAD
OneNote for AutoCAD itakuruhusu kuandika madokezo kando ya mchoro wako kutoka ndani ya AutoCAD. Hili linaongeza tija ya fundi majengo na wahandisi kote ulimwenguni kwa kutumia AutoCAD kuunda michoro ya 2D na 3D. Madokezo haya yanachelezwa na wingu na yanaweza kufikiwa wakati wowote. Watumiaji wanaweza kuona madokezo haya wakati ujao watakapofungua mchoro katika AutoCAD.
OneNote Class Notebooks
Panga taratibu zako za masomo na maudhui ya kozi katika daftari lako la dijitali pamoja na nafasi ya kazi ya binafsi kwa kila mwanafunzi, maktaba ya maudhui ya karatasi za mazoezi, na nafasi ya ushirikiano kwa masomo na shughuli za ubunifu.
OneNote Web Clipper
OneNote Web Clipper hukuwezesha kuhifadhi kurasa za wavuti kutoka kwenye kivinjari chako hadi kwenye madaftari yako ya OneNote. Kwa mbofyo mmoja tu, hukusaidia kunasa mambo haraka na kukumbuka zaidi maishani mwako.
Powerbot for Gmail
Hifadhi barua pepe, mazungumzo na viambatisho muhimu kwenye OneNote moja kwa moja kutoka kwenye kiolesura cha Gmail. Hakuna kuenda mbele au kurudi nyuma kati ya programu tena.
WordPress
Tunga machapisho yako ya WordPress kwenye kifaa chochote, kwenye mifumo yote, mtandaoni na nje ya mtandao katika OneNote na utumie kwa urahisi maudhui kutoka kwenye madokezo yako yote yaliyopo.
Zapier
Zapier ni njia rahisi sana ya kuunganisha OneNote kwa programu ambazo tayari unatumia, kama vile Salesforce, Trello, Basecamp, Wufoo na Twitter. Tumia programu hii kucheleza vidokezo, kuweka rekodi ya kazi zilizokamilika au kuhifadhi waasiliani, picha, kurasa mpya za wavuti na zaidi.